Cart

Your Cart is Empty

Back To Shop

Cart

Your Cart is Empty

Back To Shop
Sale!

Mti wa Milele by Story Moja by Wangari Grace

KSh380.00

SOMA PAMOJA NA MTOTO WAKO Furahia uhondo wa kusoma pamoja na mtoto wako.
Mtoto wako atavipenda vitabu maishani mwake na atajifundisha kwa wepesi endapo
utazingatia hoja kumi rahisi zilizoorodheshwa hapa chini.
1. Soma pamoja na mtoto wako katika mazingira yaliyotulia kama vile kwenye
chumba cha kulala.
2. Mhimize mtoto awe na mazoea ya kusoma hadithi nzima kwa kutumia
viziada vya lugha kama vile kupandisha sauti. Asome hadithi nzima kwanza
akilenga kuifurahia tu kisha aisome tena ili ajue yaliyomo.
3. Mhimize mtoto ayaashirie maneno kwa vidole hasa anaposoma hadithi
aliyokwisha kuisoma awali.
4. Chunguza kama mtoto anaelewa aliyoyasoma kwa kumuuliza maswali rahisi
kuhusu michoro, wahusika na hadithi kwa jumla.
5. Kuwa na mtazamo chanya kuhusu hatua anayopiga mtoto katika usomaji
wake. Usimvunje moyo bali umsifu kwa kila hatua anayopiga.
6. Hakikisha kwamba mtoto anaisoma hadithi mara kadhaa.
7. Baada ya mtoto kuzoea kusoma hadithi fulani, mhimize ajaribu kukusomea
baadhi ya maneno ya hadithi hiyo au hadithi nzima,
8. Mnunulie mtoto wako vitabu tofauti tofauti vya kuburudisha kama vile vitabu
vya picha, vya kuchekesha na vya kuelimisha.
9. Mwonyeshe mtoto wako kwamba una nia ya kufuatilia na kujua hadithi
anazozisoma kwa kumuuliza maswali kuhusu hadithi hizo. Pia mhadithie
hadithi ulizosoma kwenye vitabu ulivyo navyo.
10.Uwe kielelezo bora kwa mtoto wako ili avithamini vitabu. Mwache mtoto
wako akuone wewe ukisoma vitabu vingi.

 

ISBN: 9789966001726

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mti wa Milele by Story Moja by Wangari Grace”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Category:
Sale!

Cart

Your Cart is Empty

Back To Shop
Call Us